Pamoja na ushindi mkubwa wa mabao matano kwa moja walioupata dhidi ya Arsenal usiku wa kuamkia leo, mabingwa wa soka nchini Ujerumani FC Bayern Munich huenda wakaadhibiwa na shirikisho la soka barani Ulaya UEFA.
Mashabiki wa klabu hiyo wameiponza klabu hiyo na kujikuta ikiingia katika tuhuma ambazo huenda zikawaingiza katika adhabu ya kutozwa faini na shirikisho hilo la soka.
Katika mchezo wa jana uliochezwa kwenye uwanja wa Emirates kaskazini mwa jijini London, mashabiki wa Bayern alitupa makaratasi katika neo la kuchezea na kusababisha karaha kwa wachezaji na waamzui wa mchezo huo.
Kitendo hicho kilisababisha mchezo kusimamishwa kwa muda, ili kutoa nafasi kwa wafanyakazi wa uwanja kutoa makaratasi eneo la kuchezea.
Kanuni na sheria za shirikisho la soka barani Ulaya, zinakataza vitendo vya namna hiyo ambavyo mara nyingi hufanywa na mashabiki, hivyo UEFA wanatarajia kukutana na kutangaza maamuzi.