Mshambuliaji kutoka nchini Gabon Pierre-Emerick Aubameyang, ameisaidia klabu yake ya Borussia Dortmund kutinga hatua ya robo fainali ya ligi ya mabingwa barani Ulaya, baada ya kufunga mabao matatu kati ya manne kwenye mchezo wa mkondo wa pili wa 16 bora dhidi ya Benfica ya Ureno.

Katika mchezo wa mkondo wa kwanza Borussia Dortmund walikubali kupoteza kwa kufungwa bao moja kwa sifuri, na walitakiwa kusaka ushindi wa mabao mawili kwa sifuri na kuendelea ili waendelee katika michuano hiyo.

Bao lingine la Borussia Dortmund lilifungwa na Christian Pulisic katika dakika ya 59 huku Aubameyang akifungwa dakika ya 4, 61 na 85.

Ushindi huo unaiwezesha Borussia Dortmund kupita kwa jumla ya mabao manne kwa moja, na sasa inasubiri ratiba ya hatua ya robo fainali itakayopangwa na shirikisho la soka barani Ulaya UEFA baadae mwezi huu.

FC Barcelona Kiboko Yao, Yapindua Matokeo Camp Nou
Mfanyabiashara wa pombe aina ya viroba ajiua