Klabu ya LA GALAXY huenda ikaharibu mipango ya Man Utd ya kutaka kumbakiza mshambuliaji wao kutoka nchini Sweden,  Zlatan Ibrahimovic kwa kumsainisha mkataba mpya kabla ya mwisho wa msimu huu.

LA GALAXY inayoshiriki ligi kuu ya soka nchini Marekani imeonyesha dhamira ya kumsajili Zlatan mwishoni mwa msimu huu, huku ikiweka wazi dhamira ya kumlipa mshahara mkubwa kuliko wachezaji wote wanaocheza katika ligi hiyo.

Kwa mujibu wa tovuti na Sports Illustrated, LA Galaxy  wapo makini na jambo hilo na wanaamini wana uwezo wa kumshawishi mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 35, hadi akakubali kujiunga nao mwishoni mwa msimu.

Man Utd wamewahi kuthibitisha kuwa kwenye mazungumzo na Zlatan kwa ajili ya kumsainisha mkataba mpya, lakini mhusika alipohojiwa na vyombo vya habari alisema suala la kusaini ama kutosaini litafahamika mwishoni mwa msimu huu.

Zlatan alisaini mkataba wa mwaka mmoja alipojiunga na Man Utd mwanzoni mwa msimu huu akitokea kwa mabingwa wa soka nchini Ufaransa,  PSG baada ya kuwa huru.

Tanesco yatoa siku 14 kwa wadaiwa sugu kulipa deni
Simba Yamuacha Method Mwanjali