Mshambuliaji wa klabu ya Arsenal,  Alex Oxlade-Chamberlain ametajwa kuwa miongoni mwa wachezaji ambao huenda wakaondoka mwishoni mwa msimu huu, endapo Arsene Wenger ataendelea kuwa meneja wa The Gunners.

Gazeti la The Sun limemtaja mshambuliaji huyo mwenye umri  wa maika 23, kwa kueleza amechoshwa na madhila wanayoyapata katika kipindi hiki ambacho wamekua akiwambulia matokeo mabovu, yanayoendelea kuwakwamisha kwenye mipango ya kutwaa mataji.

Gazeti la The Sun limeibuka na taarifa hizo baada ya The Gunners kukubali kufungwa kwa mara ya pili mfululizo na FC Bayern Munich mabao matano kwa moja msimu huu na kutupwa nje ya michuano ya Ulaya kwa jumla ya mabao 10 kwa 2.

Wachezaji wengine wakongwe katika kikosi cha Arsenal ambao hawakutajwa na gazeti hili, inasemekana wameweka dhamira ya kushinikiza kuondoka klabuni hapo, kutokana na kutopendezwa na mbinu za meneja huyo wa kifaransa.

Mkataba wa sasa wa Chamberlain umesaliwa na miaka 18, na imethibitika hatosaini mkataba mpya endapo ataona mipango ya Wenger ya kupewa mkataba mpya inapewa kipaumbele.

Wenger atamaliza mkataba wa kukinoa kikosi cha Arsenal mwishoni mwa msimu huu, lakini kuna tetesi zinadai kuwa, tayari uongozi wa klabu hiyo umeshamuandalia mkataba mwingine wa miaka miwili.

Antonio Conte Hataki Kuremba FA Cup
Tanesco yatoa siku 14 kwa wadaiwa sugu kulipa deni