Wanachama wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Arusha wametakiwa kuwaheshimu mabalozi wa nyumba kumi wanaotokana na chama hicho ili kuleta maendeleo ya kasi na yenye tija kwa wananchi hali ambayo itaongeza idadi ya wanachama wapya
Wanachama hao wamesisitizwa kuacha majungu badala yake kuhakikisha wanaimarisha chama kwa kushirikiana na viongozi mbalimbali sanjari na kufungua matawi na kugawa kadi mpya kwa wakati.
Hayo yamesemwa na  Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Arusha, Lucia Mwiru wakati alipokuwa akizungumza na wanachama, mabalozi wa nyumba kumi, makatibu Kata, na wazee maarufu
Amesema yeye ni mgeni katika wilaya hiyo na ndio maana anapita kila Kata kwaajili ya kuongea na wanachama wa CCM ikiwemo kuhakikisha kila jambo wanalolifanya ni lazima mabalozi wa nyumba kumi waheshimiwe ikiwemo kushirikishwa katika miradi mbalimbali ya chama.
Aidha, amesema kuwa mabalozi ni watu muhimu sana katika chama hivyo wana haki ya kuhusishwa katika miradi mbalimbali ya chama ili na wao wanufaike na keki iliyopo badala ya watu wachache kukumbatia keki hiyo
Naye Katibu wa Siasa na Uenezi CCM Wilaya ya Arusha Mjini, Jasper Kishumbua ametoa rai kwa wanachama wa Chama hicho Mkoa wa Arusha na kata mbalimbali kuongeza idadi ya wanachama pamoja na kufungua matawi ili kuongeza ari katika chama
Kwa upande wa wanachama waliohudhuria katika mkutano huo  wametoa rai kwa wanachama kujua wanachama wote wanaoishi kwenye kila.

Waajiri watakiwa kuwasilisha taarifa za mapato ya wafanyakazi wao
Max Allegri Atikisa Kibiriti, Azifikiria FC Barcelena, Arsenal