Mlinda mlango wa klabu bingwa nchini Mauritius AS Port-Louis 2000 (ASPL 2000) Joseph Leopold, amezuiliwa kusafiri na kikosi cha klabu hiyo kuelekea Sudan kwa ajili ya mchezo wa 32 bora wa ligi ya mabingwa barani Afrika dhidi ya Al-Hilal, ambao utachezwa jumapili.

Mchezaji huyo ametii agizo hilo, kutokana na kesi ya dawa za kulevya inayomkabili tangu mwezi Septemba, ambapo mmlaka za kiusala nchini Mauritius zilikagua nyumbani kwake na kukuta shehena ya dawa hizo.

Amri ya kuzuia kuondoka nchini humo, ilitolea na mahakama inayosikiliza kesi yake, kwa kuhofia huenda akatoroka.

Kabla ya amri hiyo kutolewa, mwanasheria wa mchezaji huyo aliwasilisha ombi mahakamani la kutaka mteja wake kuruhusiwa kuondoka nchini Mauritius sambamba na wachezaji wenzake kwa ajili ya mchezo huo, lakini ilishindikana.

Hata hivyio mwanasheria huyo aliithibitishia mahakama kuwa, mteja wake mwenye umri wa miaka 27, akimaliza majukumu ya kuitumikia klabu yake ya ASPL 2000 katika mchezo wa ligi ya mabingwa angerejea nchini humo, lakini bado mambo yalikua magumu.

Hata hivyo hii si mara ya kwanza kwa Leopold kunyimwa ruhusa ya kutoka nje ya Mauritius, kwani mapema mwezi uliopita alikosa ruhusa ya kusafiri na wachezaji wenzake katika safari ya Kenya, ambapo walikwenda kucheza mchezo wa hatua za awali dhidi ya Tusker FC, lakini alishiriki kwenye mpambano wa mkondo wa pili ambao ulichezwa mjini Port Louis.

Katika mchezo huo ASPL 2000 walipata ushindi wa jumla wa mabao matatu kwa moja. Katika mchezo wa mkondo wa kwanza walilazimisha sare ya bao moja kwa moja wakiwa Kenya na walipopambana nyumbani walichomoza na ushindi wa mabao mawili kwa moja.

Maofisa Wa TFF Washinda Kesi Ya Rushwa
Ivan Rakitic Kubaki Camp Nou