Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheli (KKKT), Dayosisi ya Pare, Charles Mjema amewapongeza waumini wa usharika huo kwa kuongeza mapato yanayotokana na sadaka.
Askofu Mjema amesema hayo akiwa ni mgeni rasmi wa Mkutano Mkuu wa 20 wa Dayosisi ya Kaskazini uliofanyika kwenye dayosisi hiyo.
“Nimeona kwenye taarifa yenu hapa mwaka 1995 sadaka ilikuwa Sh. 9.4 milioni, lakini mwaka jana matoleo yenu kwa ajili ya kazi ya bwana yamefikia Sh412.9 milioni. Hongereni,” amesema Mjema.
Aidha, Askofu Mjema amesema wapo watu wanaoogopa kuweka malengo makubwa kwa kukosa ujasiri kutokana na kutokuwa na utamaduni wa kumtolea Mwenyezi Mungu.
Kwa upande wake, Mchungaji Kiongozi wa Usharika wa Karanga wa Moshi Mjini Dayosisi ya Kaskazini, Fred Njama amesema nchi imekumbwa na tatizo kubwa la ajira kwa vijana wanaomaliza elimu ya juu na kuishauri Serikali kuliangalia suala hilo kiundani zaidi.

Rais Magufuli awataka makatibu 'CCM' kugombea Uenyekiti
Mwalimu akamatwa na shehena ya pombe aina ya viroba