Mwenyekiti wa CCM Taifa, Dkt. Rais John Magufuli amewataka makatibu wa mikoa wa chama hicho wanaotaka kuingia katika vikao vya Halmashauri Kuu (NEC) ya Taifa ya chama hicho kugombea Uenyekiti.
Ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa kikao cha NEC Mkoani Dodoma, Dkt. Rais Magufuli amesema kuwa kuna watu wana umuhimu wa kuingia katika vikao vya Halmashauri Kuu na kwamba wakikosa kutakosekana uwakilishi .
“Nikawaambia mbona mwaka uliopita waliposimama wakimpinga mwenyekiti makatibu mlikuwepo? Wakati mwenyekiti anawalipa mshahara mbona hamkumtetea? Mbona hamkusimama kupigana na bado wakaendelea kuimba wanaimani na mtu fulani na wengine mkawamnaitikia,”amesema Dkt. Magufuli.
Hata hivyo, Rais Dkt. Magufuli amesema kuwa mabadiliko ya Katiba na Kanuni ambayo yatapunguza idadi ya wajumbe wa vikao vya juu vya chama hicho walishayajadili katika kikao kilichofanyika Desemba 13 mwaka jana, ni matumaini yake kuwa kikao hicho hakitachukua muda mrefu kuyajadili.