Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo, Florent Ibenge, amethibitisha kuondoka katika nafasi hiyo itakapofika mwaka 2018.

Ibenge ambaye alikiongoza kikosi cha Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo wakati wa fainali za Afrika za 2017 zilizofanyika nchini Gabon mwanzoni mwa mwaka huu, amethibitisha taarifa hizo kufuatia mkataba wake wa sasa kutarajia kufikia kikomo mwaka 2018.

Ibenge amesema angependa kuendelea kuwa mkuu wa benchi la ufundi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, lakini anahisi utakapowadia muda wa mkataba wake kumalizika, itakuwa ni vyema kuwaachia wengine ili waendelee kuisaidia nchi hiyo upande wa soka.

Mbali na kutoa sababu hizo, pia aliwaambia waandishi wa habari kuhusu mpango wa kuhitaji changamoto mpya katika ukufunzi wake hususan kipindi hiki ambacho anashuhudiwa akiwa na majukumu mengine ya kukinoa kikosi cha klabu ya AS Vita.

Mwishoni mwa juma lililopita, Ibenge alikuwa katika majukumu ya kukiongoza kikosi cha klabu hiyo kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa barani Afrika, ambapo AS Vita ilikuwa ugenini nchini Gambia ikicheza na Ports Authority.

Tangu mwaka 2014, kocha huyo amekuwa akifanya kazi ya kukinoa kikosi cha klabu hiyo huku akikubali kubeba mzigo wa kukiongoza kikosi cha timu ya taifa lake, ambacho katika fainali za AFCON 2017 kiliishia kwenye hatua ya robo fainali.

Pigo Man Utd, Kupambana Bila Mshambuliaji
Thesis Statement Illustrations for Research Papers