Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Nuru Millao amewataka Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini kuuza huduma zitolewazo na Wizara au Taasisi husika kwa lengo la kutekeleza shughuli za Serikali.
Ameyasema hayo mjini Dodoma katika Ukumbi wa Hazina ndogo wakati wa Kikao Kazi cha Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini kilicholenga kuwajengea uwezo Maafisa Mawasiliano Serikalini.
“Katika kikao hiki tutapata nafasi ya kujadiliana namna bora ya kuboresha mawasiliano katika maeneo yetu ya kazi, kuisemea Serikali, kuitendea haki Serikali katika kuwasilisha taarifa mbalimbali za Serikali” amesema, Millao.
Kwa upande wake Mhadhiri Msaidizi Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dotto Paul amesema kuwa wajibu mkuu wa Maafisa Mawasiliano Serikalini ni Kufuatilia kwa ukaribu nini kimeripotiwa kwenye vyombo vya habari kwa lengo la kuwa tayari kujibu au kufuatilia habari zinazohusu Serikali.
Hata hivyo, Theofil Makunga kutoka Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) akiwasilisha mada kuhusu mtazamo wa Wahariri kwa Maafisa Mawasiliano wa Serikali, amewataka Maafisa Mawasiliano kuhakikisha wanasimamia idara zao ipasavyo kwa kutoa taarifa sahihi kwani vyombo vya habari vinawategemea kwa kiwango kikubwa