Mwimbaji wa muziki wa kizazi kipya nchini, TID amesema kuwa huu sio wakati wa kukataa ukweli, wala haihitaji hata kwenda chama kingine, pia haihitaji kuwa mwanasiasa ili kukemea matumizi ya dawa za kulevya bali inahitaji kuwa mtanzania kwanza kwa sababu ni janga la Taifa.
TID amesema hayo leo Machi 15, 2017 wakati akizungumza katika hafla ya mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda ya kutimiza mwaka mmoja akiwa kama mkuu wa mkoa wa Dar es salaam.
Amesema wapo baadhi ya wasanii wengine wanaoona njia aliyopo si njia sahihi, hivyo ameeleza kuwa anapenda kuwa mfano wa mambo mazuri yanayofanyika katika mkoa wa Dar es salaam na Tanzania nzima. Bofya hapa kutazama