Roy Keane, Gwiji wa Soka aliyedumu kwa kipindi muda mrefu kwenye klabu ya Manchester United, Roy Keane amemsafisha mikono meneja wa Manchester City, Pep Guardiola na kuwashushia lawama wachezaji wa timu hiyo kwa kushindwa kutimiza ndoto yao ya kutinga fainali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya, usiku wa kuamkia leo.

Gwiji huyo mwenye tuzo kubwa 19 za Soka, amesema wachezaji wa Manchester City walionyesha udhaifu mkubwa dhidi ya wapinzani wao AS Monaco, hali ambayo ilitoa nafasi kwa wenyeji kupata nafasi ya kuchomiza na ushindi wa mabao matatu kwa moja.

Amesema hawezi kumlaumu Guardiola kufuatia kichapo hicho, bali lawama zake anazielekeza kwa wachezaji wa Man City, ambao walikua na kila sababu ya kucheza mchezo huo kwa kujituma wakati wote bila kukata tamaa.

“Wachezaji wa Man City wameonyesha udhaifu mkubwa, hawakucheza kwa kujituma wakati wote, ukiangalia safu ya ulinzi, kiungo na ushambuliaji hazikua na ushirikiano wa kutosha, AS Monaco walitumia udhaifu huo kuwashinda,” Keane aliiambia ITV.

“Nafikiri Guaradiola atakua ameona matatizo hayo, na huenda yakawa chagizo kubwa sana kwake la kufanya mabadiliko makubwa mwishoni mwa msimu huu, kwa kuwasajili wachezaji ambao wataweza kwenda sambamba na kasi ya mafundisho yake,” aliongeza.

“Huwezi kukifananisha kikosi cha Man city na FC Barcelona ama Bayern Munich ambapo Pep Guardiola aliwahi kuzitumikia, kila mmoja anatambua uwezo wa meneja huyu, hivyo ninaamini kuna mabadiliko makubwa yanakuja ndani ya miezi michache ijayo.”

Kuondolewa kwenye michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya, kunaifanya Man City kutegemea michuano ya kombe la FA, ambayo huenda ikawawezesha kumaliza msimu wakiwa na taji la ubingwa chini ya meneja huyo kutoka nchini Hispania.

Kamati Ya Serengeti Boys Yaanika Mikakati
Video: Alichosema Makene kuhusu Lissu kukamatwa na Polisi Dodoma