Shirikisho la soka duniani (FIFA) limetangaza kuifungia nchi ya Mali kushiriki michuano ya kimataifa, kwa madai ya serikali ya nchi hiyo kuingilia masuala ya soka.
Waziri wa Michezo wa Mali, Housseini Amion Guindo aliamua kuunda kamati ya muda kuendesha Shirikisho la Soka la Mali (FEMAFOOT) baada ya kuona uongozi uliokuwa madarakani haukua sahihi kwa mtazamo wa Serikali.
Lakini baada ya FEMAFOOT kufikisha malalamiko yake FIFA, shirikisho hilo la soka duniani, limeamuru serikali ya Mali, kuvunja kamati hiyo hadi Ijumaa (leo).
Baada ya kuona hakukuwa na utekelezaji hadi mishale wa saa tano na dakika hamsini na tisa (5:59) usiku, FIFA ilitangaza kuifungia Mali.
BARUA YA FIFA KWENDA FEMAFOOT |
Fatma Samoura ndiye aliyeandika barua hiyo ya kuifungia Mali kushiriki michuano iliyo chini ya FIFA, jambo ambalo bila shaka ni pigo kwa Mali.