Kikosi cha Valencia kitapambana na mabingwa wa soka nchini Hispania FC Barcelona mwishoni mwa juma hili, bila ya Luis Nani na Santi Mina ambao wanasumbuliwa na majeraha.

Mina ambaye alianza katika michezo miwili iliyopita baada ya kuwa nje ya uwanja kwa majuma matatu kufuatia majeraha ya goti, amerejea tena katika benchi la wagongwa la klabu hiyo, kutokana na maumivu wa kiazi cha mguu aliyoyapata akiwa katika maandalizi ya kuelekea kwenye mchezo huo wa jumapili.

Naye mshambuliaji wa pembeni kutoka nchini Ureno Nani anaendelea kusumbuliwa na majeraha ya paja aliyoyapata wakati wa mchezo wa ligi ya Hispania dhidi ya Real Madrid mwezi uliopita.

“Nani atamuona mtaalamu kwa ajili ya kufanyiwa vipimo kwa mara ya pili ili kujua maendeleo ya jeraha lake,” imeeleza taarifa iliyochapishwa kwenye tovuti ya klabu ya Valencia.

Mshambuliai Rodrigo Moreno anatarawajiwa kuwa sehemu ya kikosi cha Valencia, sambamba na Munir El Haddadi aliesajiliwa kwa mkopo akitokea Barca tangu mwaka 2016.

Simone Zaza, alietua klabuni hapo kwa mkopo mwezi Januari akitokea kwa mabingwa wa soka nchini Italia Juventus, naye anatazamiwa kuanza katika kikosi cha kwanza dhidi ya FC Barcelona.

Valencia ambao msimu uliopita walishinda Camp Nou, wamekua na matokeo mazuri katika michezo mitano iliyopita.

Wes Morgan: Hatuihofii Klabu Yoyote Ulaya
Lowassa Ajibu Madai ya Bulembo Kumpa Milioni 40 za Kampeni