Bei ya nyanya imetajwa kupanda kwa kiasi kikubwa huku wafanyabiashara wakieleza upatikanaji wake kuwa mgumu zaidi katika kipindi hiki.
Kufuatia hayo Dar24 imefanya mazungumzo na wafanyabiashara wa bidhaa hiyo jijini Dar es salaam ambao wamedhibitisha kupanda bei kwa bidhaa hiyo ambayo pia kwa upande wao inapatikana kwa shida sana hali inayopelekea kuuzwa kwa bei ya juu.
Akizungumzia sakata hilo, Makamu Mwenyekiti wa chama cha ushirika cha wauza mazao jumla katika soko la Ilala jijini Dar es salaam, Yassin Kivuma amesema kuwa sababu kubwa ya nyanya kupanda bei ni kutokana na wakulima wa bidhaa hiyo nchini kuwa wachache na kulima kwa kiasi kidogo kutokana na hasara walizopata katika msimu uliopita.