Vinara wa ligi kuu ya soka nchini England Chelsea, wanaamini watazipiku baadhi ya klabu za barani Ulaya katika mbio za usajili wa kiungo kutoka nchini Ufaransa na klabu ya AS Monaco, Tiemoue Bakayoko.

Gazeti la Daily Mirror limeripoti kuwa, meneja wa Chelsea Antonio Conte anaendelea kutoa ushawishi mkubwa kwa viongozi wa juu wa klabu hiyo, kuhakikisha Bakayoko anasajiliwa mwishoni mwa msimu huu.

Bakayoko, mwenye umri wa miaka 22, amekua na msimu mzuri katika ligi ya Ufaransa, na juma lililopita aliifungia AS Minaco bao muhimu dhidi ya Man City, ambalo liliivusha klabu hiyo kwenye michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya.

Conte anadaiwa alikua na mipango ya kutaka kumsajili kiungo kutoka nchini Ubelgiji na klabu ya AS Roma ya Italia Radja Nainggolan mwenye umri wa miaka 28, lakini ameonyesha kuwa na mahaba makubwa na Bakayoko.

Wakati Chelsea wakiamini watafanikiwa kumsajili kiungo huyo, klabu nyingine zinazotajwa kuwa katika mawindo makali dhidi ya Bakayoko ni Manchester United na Arsenal zote za England.

Mario Balotelli Kuhama Ufaransa?
Video: Ruge afunguka kuhusu Makonda kuvamia Clouds Media Group