Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Uganda Milutin ‘Micho’ Sredejovic ametangaza kikosi cha wachezaji 18 wakiwemo nyota Emmanuel Okwi na Juuko Murshid watakaosafiri kwenda Nairobi kwa ajili ya mchezo wa kimataifa wa kirafiki utakaopigwa Alhamisi Machi 23 kwenye uwanja wa Nyayo.

Kambi ya muda ya timu hiyo itaanza leo jioni katika hoteli ya Sky iliyopo maeneo ya Ntinda jijini Kampala kabla hawajaodoka kesho saa 3 asubuhi kwa ndege ya shirika la ndege la Kenya Airways kuelekea Nairobi.

Wachezaji wanaosakata kabumbu nje ya Uganda wataungana na wenzao jijini Nairobi wakitokea katika klabu zao akiwemo Juuko ambaye jana aliitumikia timu yake ya Simba katika mchezo wa kombe la shirikisho dhidi ya Madini wakiibuka na ushindi wa bao 1-0.

KIKOSI KAMILI

Makipa:

Benjamin Ochan (KCCA), Isma Watenga (Vipers)

Mabeki:

Nico Wakiro Wadad (Vipers), Timothy Denis Awanyi (KCCA), Habib Kavuma (KCCA), Murshid Juuko (Simba, Tanzania), Shafiq Batambuze (Tusker, Kenya), Godfrey Walusimbi (Gor Mahia, Kenya)

Viungo:

Hassan Wasswa Mawanda (Nijmeh, Lebanon), Kirizestom Ntambia (Jimma Aba Buna), Yassar Mugerwa (Saint George, Ethiopia), Moses Waiswa (Vipers), Muzamil Mutyaba (KCCA), Joseph Ochaya (KCCA), Brian Majwega (KCCA)

Washambuliaji:

Geofrey Sserunkuma (KCCA), Emmanuel Okwi Arnold (SC Villa), Milton Karisa (Vipers)

Video: JPM amkingia kifua Makonda, Lowassa 'atolewa uvivu' na UVCCM
Mpinzani Wa Yanga Kujulikana Leo