Meya wa jiji la Dar es salaam, Isaya Mwita leo Machi 21, 2017 ameondoka nchini kuhudhuria mkutano wa siku tatu wa Serikali za mitaa Duniani (ICLEI) utakaofanyika nchini Afrika Kusini kesho Machi 22, 2017.

Mkutano huo utahusisha Mameya wote wa Afrika na utajikita katika kushugulikia mabadiliko ya tabia ya nchi pamoja na kuhakikisha matumizi mazuri ya utumiaji wa rasilimali za nchi, pia mkutano huo utajadili mabadiliko ya tabia ya Nchi, ambapo watajikita zaidi katika kujikinga na majanga ya mafuriko pamoja na kutafuta suluhisho la matatizo ya maji kwenye majiji.

Kufuatia jiji la Dar es Salaam kuwa miongoni mwa majiji ambayo hukumbana na changamoto ya mafuriko, Meya Mwita atawasilisha mada inayohusiana na kuondokana na tatizo hilo katika jiji la Dar es salaam kupitia vyanzo vya maji ikiwemo Ruvu chini, Kimbiji pamoja na vyanzo vingine ili kupitia mkutano huo kuwasaidia wakazi wa jijini la Dar es salaam kuondanokana na changamoto hiyo.

Aidha, Meya Isaya  atawasilisha mada kuhusiana na mafuriko ambapo katika mkutano huo wote kwa pamoja watajadili pamoja na kujengewa uwezo katika kuendesha majiji yao sambamba na kukabiliana na  majanga yaliyopo.

Majaliwa atembelea kiwanda cha sukari cha Alteo Mauritius
Majaliwa atembelea kiwanda cha sukari cha Alteo Mauritius