Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto. Dkt. Hamis Kigwangalla ametoa sababu za kutotaja hadharani orodha ya majina ya watu wanaojihusisha kufanya mapenzi ya jinsia moja.
Amesema hakuweza kuyataja hadharani majina hayo kwa kuwa alisikiliza ushauri aliopewa na jamii inayomzunguka.
“Mimi nashaurika, sikuweka majina hadharani kwa sababu nashaurika, listi ya watu ninayo na tunachukuwa hatua kimya kimya hili ni kosa la jinai na mtu anayekutwa na hatia anafungwa kifungo cha miaka 30 jela” Amesema Dkt. Kigwangalla
Ameyasema, hayo wakati wa maadhimisho ya siku ya Ustawi wa Jamii Duniani ambayo kitaifa imefanyika jijini Dar es Salaam, amesema kuwa kufanya mapenzi ya jinsia moja ni kosa kibaiolojia na hairuhusiwi mtu kuvutiwa na mtu wa jinsia yake.
Aidha, amesema katika sheria iliyotungwa mwaka 2012 ya kukazia adhabu ya mapenzi ya jinsia moja, kuna kipengele kinachotaka mtu achukuliwe hatua endapo ikithibitika amekaa mitindo isiyoeleweka na ikabainika kuwa ana muonekano wa watu wa aina hiyo, atafunguliwa mashtaka mara moja.
Hata hivyo, Kigwangalla amewaonya wanajihusisha na mapenzi ya jinsia moja na kusisitiza kwamba Serikali itawachukulia hatua kimya kimya.

Serikali yapigilia msumali uzalishaji wa pombe aina ya viroba
Majaliwa atembelea kiwanda cha sukari cha Alteo Mauritius