Mshambuliaji wa klabu ya Galatasaray Lukas Josef Podolski usiku wa kuamkia leo alistaafu kuichezea timu yake ya taifa ya Ujerumani kwa heshima, baada ya kufunga bao pekee na la ushindi katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya England.

Podolski ambaye alikua akicheza mchezo wake wa 130, alifunga bao hilo katika dakika ya 69 kwa shuti kali ambalo lilimshinda mlanda mlango wa England Joe Hart.

Mshambuliaji huyo anastaafu soka upande wa timu ya taifa ya Ujerumani, baada ya kuitumikia tangu mwaka 2004 na alikua sehemu ya kikosi cha timu hiyo kilichotwaa ubingwa wa kombe la dunia mwaka 2014 huko nchini Brazil.

Mbali na sifa ya kutwaa ubingwa wa dunia, Podoski alichangia mafanikio ya Ujerumani ya kufika kwenye hatua ya nusu fainali ya michuano ya Ulaya (Euro) mwaka 2010, 2008, 2012 na 2016.

Kabla ya mchezo wa jana ambapo Podolski alifunga bao lake la 49, mashabiki wa Ujerumani walionyeha heshima kubwa kwa mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 31 kwa kuvaa flana zenye picha na jina lake, hali ambayo ilionyesha kumpa heshima wakati wote wa mchezo.

Podilski ataendelea kucheza soka upande wa klabu na tayari imeshathibitika atajiunga na klabu ya Vissel Kobe ya nchini japan mwishoni mwa msimu huu, akitokea Galatasaray ya Uturuki.

Klabu nyingine alizowahi kuzitumikia ni FC Köln II (2003–2006), Bayern Munich (2006–2009),       FC Köln 88 (2009–2012), Arsenal (2012–2015) na  Inter Milan (2015).

HBOs VICE spreads misinformation about biotechnology
JPM amteua Mwakyembe kuwa Waziri wa Habari