Bosi wa kikosi cha Atletico Madrid Diego Simeone ameapa kutofikiria kufanya kazi na mahasimu wake Real Madrid, baada ya kuulizwa kama ana mpango huo kwenye maisha yake.

Simione amesema suala hilo haliwezi kutokea na wala hafikirii kujihusisha na klabu hiyo kutokana na kufahamu kuwa, haiwezekani kwa viongozi wa Real Madrid kumfikiria mtu kama yeye kwa kumkabidhi benchi la ufundi.

Gwiji huyo wa soka kutoka nchini Argentina mwenye umri wa miaka 46, tayari ameshaiwezesha Atletico Madrid kufikia malengo makubwa ya kutwaa mataji ya ligi ya nchini Hispania (La Liga), Kombe la Mfalme (Copa del Rey), kombe la Hispania (Supercopa de EspaƱa) pamoja na kufika hatua ya fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya mara mbili.

“Haitatokea mimi kwenda kufanya kazi upande wa pili wa mji wa Madrid,”

“Kimantiki haiwezekani hata kidogo jambo hilo kutokea kwenye mchezo wa soka, hata viongozi wa Real Madrid wanajua hawawezi kunifuata na kuzungumzia suala la kunipa ajira.

“Naamini ikitokea ninaondoka hapa nitapata mahala pengine pa kufundisha soka, kutokana na umri wangu kunuruhusu kufanya kazi hii, lakini sio kwenda Real Madrid.

Swali kwa Simione kuhusu kufikiria kufanya kazi na Real Madrid katika maisha yake ya ukufunzi wa soka, lilikuja kufuatia mkataba wake na klabu ya Atletico Madrid kutarajia kufikia kikomo mwishoni mwa msimu huu.

Hatma Ya Ozil, Sanchez Kujulika Mwezi Mei
Majaliwa atembelea kiwanda cha nguo Mauritius, akaribisha wawekezaji kuja Tanzania