Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli leo Machi 24 anawaapisha mawaziri wawili aliowateua jana Machi 23, ambapo itatangulia hafla ya kuwaapisha mabalozi wa nchi za nje nchini Tanzania.

Rais Magufuli amefanya mabadiliko madogo katika Baraza la Mawaziri ambapo amemteua Dkt. Harrison George Mwakyembe kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo. Nape Moses Nnauye ndiye aliyekuwa anashikilia wadhifa huo.

Aidha, Dkt Magufuli amemteua Prof Palamagamba Aidan John Mwaluko Kabudi kuwa Waziri wa Katiba na Sheria.
Mawaziri hao wanaapishwa Ikulu ya Magogoni, jijini Dar es Salaam

Mbunge ang'atuka kugombea nafasi hii ndani ya CCM
Video: JPM atinga tena bandarini Dar, Wanywaji viroba waipongeza Serikali