Pamoja na taarifa kueleza kuwa, kiungo wa vinara wa ligi ya Ufaransa AS Monaco Tiemoue Bakayoko yupo katika mipango ya kusajiliwa na klabu ya Chelsea wa England, uongozi wa Man Utd umeanza mikakati ya kuvuruga dili hilo.
Jana baadhi ya vyombo vya habari vya England viliripoti kuwa, Chelsea wamefikia pazuri katika harakati za kumsajili kiungo huyo, na huenda akaondoka mara baada ya msimu huu kumalizika.
Mapema hii leo Man utd wametajwa kuingia kati mpango wa usajili wa Bakayoko, baada ya kuwatuma wasaka vipaji wake nchini Ufaransa kumgutilia kwa ukartibu kiungo huyo, ambaye aliipeleka AS Monaco kwenye hatua ya robo fainali ya ligi ya mabingwa barani Ulaya kwa kufunga bao tatu katika mchezo wa mkondo wa pili uliomalizika kwa AS Monaco kuibuka na ushindi wa mabao matatu kwa moja dhidi ya Man City.
Hata hivyo Bakayoko, bado ana mkataba wa kuitumikia AS Monaco hadi mwaka 2019, na huenda hatua hiyo ikaendelea kuikuza thamani yake katika kipindi cha usajili wa majira ya kiangazi.