Ndege ndogo ya shirika la ndege la Msumbiji imeanguka na kusababisha vifo vya watu watano, katika mpaka wa Msumbiji na Zimbabwe.
Ndege hiyo ilikuwa na abiria wanne na wafanyakazi wawili, ilikuwa ikisafiri kutoka jiji la Beira kwenda Mutare kupitia eneo la mashariki kwenye mpaka wa Msumbiji na Zimbabwe.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Maputo, Mkurugenzi wa Mamlaka ya Anga ya Msumbiji, Joao de Abreu alisema kuwa bado wanaendelea kuafanya uchunguzi kuhusu chanzo cha ajali hiyo na kuthitibisha kuwa kwa mujibu wa taarifa za awali walizozipata, mtu mmoja amenusurika.
Hata hivyo, Mkurugenzi huyo wa Mamlaka ya Anga alieleza kuwa hali ya hewa inaweza kuwa sehemu ya chanzo cha ajali hiyo mbaya.
Kwa mujibu wa IACM, ndege hiyo ilibeba vigogo wa kampuni maarufu ya Cornelder ambayo ni kampuni binafsi inayomiliwa na raia wa Uholanzi kwa ubia na raia wa Msumbiji.