Kiungo wa Tottenham Hotspurs Erik Lamela atakosa sehemu ya msimu wa 2016/17 iliyosalia, kufuatia majeraha ya paja yanayomkabili kwa zaidi ya miezi minne.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 25, ameshindwa kujumuika na wachezaji wenzake tangu mwezi Oktoba mwaka 2016, na mwishoni mwa juma hili atafanyiwa upasuaji.

Lamela raia wa Argentina alitarajiwa huenda angerejea uwanjani miezi kadhaa baada ya kuumia, lakini mambo yaliendelea kuwa magumu, huku  akifanyiwa uchunguzi wa mara kwa mara hadi iliposhauriwa afanyiwe upasuaji hapo jana.

“Nimejitahidi kadri niwezavyo ili niweze kurejea uwanjani kwa wakati, lakini nimeshindwa kufikia lengo, nimepatiwa matibabu ambayo niliamini yangenisaidia ila hali halikua hali, sina budi kukubali ushauri wa kufanyiwa upasuaji ” Alisema Lamela kupitia televisheni ya Spurs.

“Nimejaribu kila kitu kwa misingi ya ushauri wa kitabibu, nimefanya mazoezi mepesi kwa muda niliopangiwa lakini bado sijawa fit kwa asilimia 100,” Ameandika Lamela kwenye ukurasa wake wa Tweeter.

Kwa msimu huu Lamela amecheza michezo 14 pakee, na alitarajiwa kuwa sehemu ya mipango ya kuisaidia Spurs kufikia lengo la ushindani chini ya meneja Mauricio Pochettino.

Alisajiliwa na Tottenham akitokea nchini Italia katika klabu ya AS Roma  mwaka 2013, na amekua na maendeleo mazuri ya kucheza soka lake huku akifungia 13 mpaka sasa.

Spurs wapo katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi ya England, wakiachwa point 10 dhidi ya Chelsea, pia wamefanikiwa kutinga kwenye hatua ya nusu fainali ya kombe la FA ambapo wamepangiwa kucheza na The Blues.

Azam, Ndanda Kombe La Shirikisho La ASFC 2016/2017
Wanafunzi wasumbuliwa na mapepo shuleni