Nchi wanachama wa Umoja wa Afrika Mashariki pamoja na Sektarieti ya Umoja huo (EAC) wamehimizwa kuharakisha mchakato wa kuhakikisha kada zingine za afya ikiwemo ya uuguzi na kada nyingine zenye sifa  na viwango vinavyofanana na madaktari kuajiriwa kwenye nchi yeyote ya Afrika Mashariki

Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamiii, Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ambaye ni Mwenyekiti wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Afya wa Afrika mashariki kwenye kikao cha 14 kinachofanyika nchini Burundi.

Ummy amesema amefurahishwa sana na hatua iliyofikiwa na  nchi wanachama wa Jumuiya hiyo ambapo hivi sasa madaktari wanaotoka katika jumuiya hiyo kuajiriwa

Aidha, amesema kuwa kikao hicho kimejadili kuhusu kuimarishwa kwa mafunzo na usimamizi wa pamoja  wa wataalam wa afya, udhibiti wa magonjwa ya milipuko pamoja na magonjwa ya kuambukiza kama vile Ebola, Mafua makali ya ndege, Kifua Kikuu(TB) na Ukimwi.

“Bado Afrika Mashariki hatufanyi vizuri katika afya ya uzazi na mtoto na hivyo kusababisha kutofikia malengo ya kidunia ya Millenia yaliyowekwa,hivyo tuongeze jitihada katika hili”,amesema Waziri Ummy.

Wakati huo huo Waziri Ummy akiwa nchini humo ameshiriki uzinduzi wa kongamano la Kimataifa la afya ya Sayansi lililofunguliwa na Rais wa Burundi, Piere Nkurunzinza ambalo limeandaliwa na Kamisheni ya Utafiti wa Masuala ya Afya ya Jumuiya ya Afrika Mashariki

Kongamano hilo la siku tatu lina lengo la kujadili  na kujipanga katika kukabiliana na majanga ikiwemo ya magonjwa mapya yanayojitokeza(Emerging Diseases) na yale yanayojirudia (Re-emerging Diseases) na linawawashirikisha wataalam wa afya na watafiti kutoka nchi mbalimbali.

Taarifa Ya Maendeleo Ya Ukarabati Wa Uwanja Wa CCM Kirumba, Mwanza
Azam, Ndanda Kombe La Shirikisho La ASFC 2016/2017