Ziara ya Waziri Mkuu wa Ethiopia hapa nchini imetoa changamoto kubwa kwa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano kuliagiza Shirika hilo kuweka mikakati madhubuti ya kuzalisha na kuuza umeme kwa bei nafuu.

Rais Dkt. Magufuli ametoa agizo hilo Jijini Dar es salaam wakati wa mazungumzo na Waziri Mkuu wa Ethiopia, Hailemariam Desalegn ambaye yuko hapa nchini kwa ziara ya kikazi ya siku mbili, amesema kuwa Waziri Mkuu wa Ethiopia ameahidi kuipatia Tanzania umeme megawati 400 kwa ajili ya kusambaza nchini.

Aidha, Desalegn amesema kuwa atatoa ofa ya megawati 400 kwa ajiri ya kusambaza nchi nzima, kwani Ethiopia umeme unauzwa kwa bei ndogo ya senti sita, hali ambayo ilipelekea kwaRais Magufuli kuliagiza Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kujifunza kile ambacho Ethiopia inafanya ili waweze kuzalisha umeme wa bei nafuu.

“Hii itakuwa ni hatua nyingine ya Tanesco kujifunza namna Ethiopia wanavyozalisha umeme na kuuza kwa bei nafuu na wao waanze kufanya hivyo,”amesema Rais Magufuli.

Hata hivyo, katika hatua nyingine Rais Magufuli amesema kuwa Waziri Mkuu wa Ethiopia ameahidi kufungua ubalozi hapa nchini na kuahidi kumpa eneo Mjini Dodoma.

 

 

Video: HipHop 6 mpya na kali
Makala: Mwakyembe Tusaidie Kuutafuna Mfupa huu, Ni Zaidi ya Bifu ya Diamond na Ali Kiba