Katika kuhakikisha suala la usalama linapewa kipaumbele, Kamishna wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam, Simon Sirro amesema kuwa ataendelea kuiweka Dar es salaam katika mikono salama.

Ameyasema hayo wakati wa ziara yake aliyoifanya Makao Makuu ya Kikosi Cha Kuzuia Ghasia (FFU) katika Kanda hiyo yaliyoko Ukonga Jijini Dar es salaam.

Amesema kuwa lengo la ziara hiyo ni kukagua magari, gwaride na zahanati ya FFU iliyoko Ukonga na kuwatahadharisha wahalifu wote kuacha mara moja mipango yao.

“Fujo siku zote huwa hazipigi hodi, hivyo ni vyema wakati wote kuwa tayari ndiyo maana tunafanya ukaguzi kwenye kikosi chetu,”amesema Sirro.

Aidha, ameongeza kuwa atahakikisha anamfuatilia Askari aliyeruhusu raia wenye asili ya Asia kulipua fataki kwa zaidi ya nusu saa kitu ambacho kilisababisha usumbufu kwa wananchi.

Hata hivyo, amesema kuwa kulipua fataki hewani bila kibali cha Polisi ni kosa kisheria  na hatua zinapaswa kuchukuliwa.

 

Treni ya kisasa yazinduliwa, kuanza safari zake Afrika Mashariki
Magazeti ya Tanzania leo Aprili 5, 2017