Wananchi wametakiwa kuwa kichocheo cha Miradi ya Maendeleo katika maeneo yao bila kujali misingi na tofauti ya itikadi zao za vyama.

Hayo yamesemwa na Mbunge wa Jimbo la Kishapu Mkoani Shinyanga, Suleiman Nchambi (CCM), alipokuwa akiongza Kikao cha  Kamati ya Mfuko wa Jimbo kilichofanyika katika Wilaya ya Kishapu ambapo jumla ya sh. milioni 82 zinatarajiwa kutolewa kwa ajili ya shughuli za maendeleo.

Amesema kuwa viongozi wa ngazi za kata wakiwemo madiwani na watendaji wana nafasi kubwa ya kuhamasisha wananchi wao kushiriki katika shughuli za maendeleo na kutoa elimu kuhusu fedha za mfuko huo.

Aidha, Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Stephen Magoiga ameitaka Kamati hiyo kuwa makini katika kusimamia fedha za mfuko wa Jimbo.

Hata hivyo, Mkurugenzi  amewataka kuendelea kushiriki katika shughuli za maendeleo na kuwa Serikali itawasaidia pale ambapo watakuwa wameibua miradi ikiwemo kuanzisha majengo ya huduma za kijamii.

 

Stendi ya Mbagala Rangitatu yageuka kuwa dimbwi
Kasesela: Serikali haiamini ushirikina, wananchi badilikeni