Nyota wa Klabu ya Real Madrid ya Hispania, Cristiano Ronaldo jana ameiongoza timu hiyo kupata ushindi ugenini kwa kuichapa magoli 2-1 timu Bayern Munich ya Ujerumani.

Katika mchezo huo mkali na wa kusisimua uliovuta hisia za wengi, ulichezwa katika dimba la Arena lililoko jijini Munich nchini Ujerumani.

Aidha, Ronaldo amemaliza ukame wa miezi saba kwenye ligi hiyo ya mabingwa Barani Ulaya wa kutofunga magoli baada ya jana kupachika magoli mawili katika mchezo ambao Real Madrid iliibuka na kidedea dhidi ya Bayern Munich.

Aidha, Ronaldo amefikisha magoli 100 na kuendelea kuwa kinara wa ufungaji katika ligi ya mabingwa Barani Ulaya.

Bao pekee la Bayern lilifungwa na kiungo, Arturo Vidal na baadaye kukosa mkwaju wa penati walioupata baada ya kupaisha.

Katika mchezo huo uliokuwa na presha kubwa mchezaji wa Bayern Munich, Javi Martinez alizawadiwa kadi mbili za njano ambazo zilizaa kadi nyekundu.

Hata hivyo, timu ya Bayern ilionekana kutoelewana uwanjani mara baada ya mchezaji wao kuzawadiwa kadi nyekundu, hali ambayo iliwapa nafasi timu ya Real Madrid kupachika magoli mawili.

 

Ronaldo Aendelea Kutesa Ulaya, Amgalagaza Messi
Live: Yanayojiri Bungeni Dodoma leo Aprili 13, 2017 muda huu