Baadhi ya Wananchi wa Mkoa wa Dodoma ambao wamekuwa ni watumiaji wakubwa wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) wameupongeza mfuko huo baada ya kuonyesha mafanikio makubwa katika utoaji huduma kwa watoto walio chini ya umri wa miaka 18.

Aidha katika hatua nyingine, wananchi hao wamesema kuwa uboreshaji wa huduma za matibabu uliofikiwa na Mfuko huo kwa sasa unatoa hamasa kwa Watanzania kujiunga na huduma zake na kunufaika nazo.

Wameyasema hayo kwa nyakati tofauti tofauti mjini Dodoma wakati wa maonyesho ya Mifuko ya Uwezeshaji ambayo yamezinduliwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ambayo yatahitimishwa  Aprili 22, mwaka huu.

“Tunawapongeza sana hasa kwakuwa na madirisha mengi ambayo yanawawezesha wananchi kujiunga na kutumia huduma hii ya Mfuko wa NHIF,”amesema Sebastian Kingu.

Aidha, mmoja wa wanachama waliotembelea banda la Mfuko, Prisca Peter amesema kuwa mfuko huo umekuwa ni Mkombozi wa afya za wananchi.

Kwa upande wake, Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu, Antony Mavunde amesema kuwa lengo la Serikali ni kuhakikisha wananchi wote wanafikiwa na huduma kupitia Bima za Afya.

Hata hivyo, Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya umekuwa ukishiriki shughuli mbalimbali zinazofanyika kwa wananchi kwa lengo la kuwafikia Watanzania wengi na kutoa huduma bora ya matibabu.

 

Majaliwa awataka wananchi kufichua uhalifu nchini
Marekani yaigeukia Iran, ni kuhusu silaha za nyuklia