Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa amewataka mabalozi wa Tanzania wanaoenda kuiwakilisha Tanzania katika nchi mbalimbali kuhakikisha wanaimarisha uhusiano na kujenga urafiki katika nchi wanazowakilisha kwa lengo la kuitangaza Tanzania kiuchumi, ikiwa ni pamoja na kueleza fursa za uwekezaji zilizopo nchini.

Mabalozi wa Tanzania walioteuliwa hivi karibuni na rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania, kuwakilisha Tanzania nnje ya Nchi, ambapo wamefika ofisi ya Waziri Mkuu mjini Dodoma kwa lengo la kumuaga na kwenda kuanza majumukumu yao katika nchi walizopangiwa.

Majaliwa amewaleza mabalozi hao kuwa Tanzania inazo fursa nyingi za uwekezaji na jukumu lao la kwanza nikuzitangaza ili kuleta wawekezaji wengi Tanzania.

TFF Yamfungia Manara, Yamlima Faini Mamilioni
Uchumi wa Zanzibar wazidi kuimarika