Waandishi wa habari nchini wametakiwa kutumia taaluma yao vizuri wawapo kazini ili kuweza kuepukana na majanga ambayo yanaweza kutokea
Hayo yamesemwa na Makamu wa Rais wa UTPC, Jane Mianji alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam kuelekea siku ya Maadhimisho ya Uhuru wa Habari Duniani,
Amesema kuwa maendeleo ya demokrasia hayawezi kuwepo bila ya kuwa na uhuru wa vyombo vya habari kwakuwa Tasnia ya habari ni nyeti duniani kote hivyo inatakiwa kuheshimiwa.
Aidha, Maadhimisho ya Uhuru wa Habari Duniani yanatarajiwa kufanyika Mei 2, 2017 hadi 03, 2017 Jijini Mwanza ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli
Maadhimisho hayo yanalenga kufikia makubaliano ya kitaifa ya kuanzisha utaratibu wa usalama na ulinzi kwa wanahabari na wafanyakazi wa vyombo vya habari, kutetea sera na mfumo wa mageuzi ya Kisheria kwa ajili ya vyombo vya habari na maendeleo endelevu.
Hata hivyo, Tukio hilo limeandaliwa kwa pamoja na MISA Tawi la Tanzania, UNESCO, Baraza la Habari Tanzania(MCT), Taasisi ya Vyombo vya Habari Tanzania (TMF), (UTPC), (MOAT), Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), (TAMWA) Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Mwanza