Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetangaza kuwepo kwa nafasi wazi ya mbunge wa viti maalumu kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kufuatia kifo cha mbunge wa viti maalum wa chama hicho, Dkt. Elly Macha.
Taarifa hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa NEC, Jaji Semistocles Kaijage ambapo ameeleza kuwa kwa mujibu wa sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai ameijulisha NEC kuhusu kuwepo kwa nafasi wazi ya Mbunge huyo.