Rais wa klabu ya Simba Evans Aveva amesema haikuwa haki kwa Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la mpira wa miguu (TFF) kumfungia msemaji wa klabu hiyo Haji Sunday Manara, bila kumpa nafasi ya kumsikiliza kutokana na kupata dharura.

Aprili 23 Kamati hiyo chini ya Makamu Mwenyekiti wake wakili Jerome Msemwa ilimfungia Manara mwaka mmoja na faini ya shilingi milioni tisa kwa kosa la kutamka maneno yasiyo na staha kwa viongozi wa Shirikisho hilo.

Aveva alisema hakukuwa na uharaka wa kutoa hukumu hiyo bila ya kumsikiliza msemaji huyo kwa kuwa klabu ilipeleka barua TFF kuomba hukumu isogezwe mbele kwani Manara alikuwa nje ya mji akishughulikia mambo yake.

“Hili suala kama uongozi wa Simba limetushangaza sana. Hatukuona sababu ya Kamati ya nidhamu kuwa na uharaka wa kiasi hicho kutoa hukumu pasi na kumsikiliza mshitakiwa ambaye klabu ilikuwa imemtolea udhuru.

“Kuna mambo mengi yanachelewa kutolewa maamuzi lakini suala la Manara aliyekuwa akiitetea klabu yake limeamuliwa haraka bila hata kumsikiliza mshitakiwa,” alisema Aveva.

Aidha Rais huyo alisema wamesikia fainali ya michuano ya kombe la FA itanyika katika uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma ambapo kwa upande wao wamesema kwa ukubwa wa mshindano hayo yalipaswa kufanyikia uwanja wa Taifa ila hawana kipingamizi na maamuzi ya TFF.

Video: Lipumba anena mazito kuhusu Maalim, amtaka aache usultani
Kinda La Chelsea Laibeba Ajax Amsterdam