Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amefanya ziara ya ukaguzi wa mradi wa maji unaojengwa jijini Dar es salaam kwa ajili ya kuwakomboa wananchi wa mkoa huo na tatizo la maji.
Amesema kuwa kukamilika kwa mradi huo utakuwa umesaidia kwa kiasi kikubwa kuondoa tatizo ambalo limekuwa likiwasumbua wakazi wa jiji la Dar es salaam.
“Kwanza kabisa naomba niwashukuru wafanyakazi wa Dawasa kwa kufanya jitihada za kutatua changamoto ya uhaba wa maji katika jiji la Dar es salaam, kukamilika kwa mradi huu kutafanikisha kuondoa kero ya maji,”amesema Makonda.
Hata hivyo, ameongeza kuwa Serikali bado inashirikiana na Exim Bank kutafuta shilingi milioni 300 kwa ajili ya kutatua kero hiyo.