Mshauri mwelekezi wa Kampuni ya SANA Gems, Gregory Kibusi ameiomba Serikali kuendelea kutoa elimu ya uchimbaji bora na uhifadhi wa mazingira kwa wachimbaji wadogo wadogo wa madini nchini.

Ametoa ombi hilo wakati wa maonyesho ya 6 ya Kimataifa ya Madini ya Vito, yaliyofanyika Jijini Arusha ambapo ameiomba Serikali kuendelea kutoa elimu hiyo ya uchimbaji bora wa madini.

Aidha, Kibusi ameongeza kuwa, ushiriki wa wachimbaji wadogo wadogo katika maonyesho hayo ni fursa kwao wa kujenga mtandao wa kibiashara  na wanunuzi hivyo kuiomba serikali kuendelea kuwahamisha wachimbaji wadogo nchini kushiriki katika maonyesho hayo.

“Nikiwa pia kama Katibu Mkuu wa wachimbaji wadogo Shinyanga, natoa wito kwa wachimbaji nchini kutumia vyama vyao washiriki maonyesho haya ya Arusha kwa kuleta madini yao. Soko la uhakika lipo,” alisema Kibusi.

Hata hivyo, Mkurugenzi wa Kampuni hiyo, Ravi Hasmukh, amesema kuwa, kampuni hiyo imeshiriki maonyesho hayo ili kuweza kujenga mtandao wa kibiashara ikiwemo pia kutoa fursa kwa Watanzania kujifunza.

Aidha, ameitaka Serikali ifikishe umeme  katika eneo hilo na  maeneo mengine mbapo shughuli za uchimbaji mdogo zipofanyika ili kuwezesha kuharakisha maendeleo ikiwemo kuwezesha shughuli za kiuchumi   na kupanua wigo wa ajira.

Maonyesho ya 6 ya Kimataifa ya Vito Arusha yalifunguliwa rasmi tarehe Mei 3 na Mkuu wa Mkoa wa Manyara Dkt. Joel Bendera na kufungwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo

Video: Makamu wa Rais atoa wito kufuatia vifo vya wanafunzi 33
Manny Pacquiao ‘ambishia tena’ Mayweather