Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa wawili wakiwa na vipande sita vya meno ya Tembo katika maeneo ya Chanika Zingiwa nje kidogo ya jijini la Dar es salaam.

Hayo yamesemwa na Kamishna wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, Simon Sirro alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, amesema kuwa watuhumiwa hao wa meno ya Tembo walikamatwa wakiwa wameyaficha katika begi dogo lililokuwa limefichwa kwenye nyasi.

“Watuhumiwa tuliowakanmata ni Senei Abbas mfanyabiashara na mkazi wa Buguruni na mwingine ni Juma Kong’wa fundi ujenzi mkazi wa Gongo la Mboto, kila siku tumekuwa tukiwaasa wananchi kuacha kujishughulisha uhalifu lakini wanaona kama tunatania, sisi popo0te walipo wahari tutkula nao sahani moja,”amesema Sirro.

Hata hivyo, ameongeza kuwa Jeshi hilo linawashikilia watuhumiwa wengine watatu kwa kosa la uvujishaji wa mithani ya kidato cha sita katika shule ya Sekondari Chang’ombe iliyopo jijini Dar es salaam.

Magazeti ya Tanzania leo Mei 11, 2017
?Live: Yanayojiri Bungeni uchaguzi wa wabunge wa Chadema EALA