Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli ameridhia maombi ya kuacha kazi kwa viongozi watatu akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Saidi Meck Sadiki.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ikulu, Katibu Mkuu Kiongozi, Mhandisi John Kijazi amesema kuwa Rais Magufuli pia ameridhia ombi la kuachia ngazi ya uongozi la aliyekuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria, Aloysius Mujulizi.

Aidha, mwingine aliyeomba kuachia ngazi na kukubaliwa ni aliyekuwa Jaji wa Mahakama Kuu Tanzania, Upendo Msuya.

Taarifa hiyo ya Ikulu imeeleza kuwa ridhaa ya maombi ya viongozi hao ilianza rasmi jana, Mei 15.

Chuo Kikuu cha Dar es salaam kuburuzwa kortini
?Live: Yanayojiri Bungeni Dodoma leo Mei 16, 2017