Mtoto Esther Wambura ambaye amenusurika kuolewa akiwa na umri mdogo, amesimulia mambo aliyofanyiwa na baba yake mzazi wakati akilazimishwa kuolewa na mtu mwenye umri mkubwa sana hali yeye ni mtoto na bado anasoma.
Esther ambaye kwa sasa analelewa na Mwalimu, Bi Palangyo baada ya kutoroka asiolewe na kukimbilia shuleni ili aendelee na masomo yake anayoamini kuwa ndiyo msaada pekee katika maisha yake, amesimulia mkasa huu wakuhuzunisha akiwa na majonzi makubwa kwa maisha anayopitia.
“Kwakweli nilifikia hatua ya kukata tamaa, nilijiona sina thamani tena hapa duniani, baba yangu mzazi anataka niolewe, nilijiuliza haki yangu ya msingi iko wapi, niliiona dunia ni chungu, ila kwa sasa ninalelewa na mwalimu,”amesema Esther
Naye Bi Palangyo amesema ameshuhudia jinsi mwanafunzi wake alivyokuwa akishuka kitaaluma hali ambayo imemshanganza na kupelekea kuanza kumfuatilia hadi kugundua unyanyasaji aliokuwa akifanyiwa na mama yake mdogo mara baada ya kutoroka kijijini ili arudi kuendelea na masomo yake.
Baada ya kugundua hali ya mtoto huyo, Bi Palangyo aliamua kumsaidia na ili kufikisha ndoto zake na kumtoa kwenye mateso anayopata kwani anauwezo mkubwa darasani. Bofya hapa kufuatilia MKASA huu wa kuhuzunisha wa mtoto Esther. Kwa mawasiliano na Bi Palangyo mwalimu anayemlea mtoto piga 0716 134 375 ili kuwasehemu ya kufanikisha ndoto za Esther katika elimu yake.