Wamiliki wa shule binafsi Jijini Arusha na waandishi wa habari kumi pamoja na Meya wa jiji hilo waliokuwa wameenda kutoa rambirambi katika shule ya msingi Lucky Vincent wamefikishwa kituo cha Polisi kwa kosa la kufanya mkusanyiko bila kibali.

Waandishi hao pamoja na wamiliki wa shule binafsi wamefikishwa katika kituo hicho huku ulinzi mkali ukiwa umeimarishwa katika kituo hicho ili kuweza kuzuia genge kubwa la watu ambalo limekusanyika kwa ajili ya kushuhudia kinachoendelea.

Aidha, miongoni mwa wanaoshikiliwa na jeshi hilo la polisi mkoani Arusha ni pamoja na Meya wa jiji hilo, Kalisti Lazaro ambapo mpaka sasa bado haijajulikna ni kipi kinachoendelea kituoni hapo.

Shirikisho la wakuu wa Polisi SADC kukutana jijini Arusha
Hali yazidi kuwa tete Kibiti, mwingine auawa kwa kupigwa risasi