Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage amesema kuwa Serikali inafanya kazi kwa mawasiliano na ushirikiano katika kuwezesha kuwavutia wawekezaji kuja kuwekeza nchini.
Ameyasema hayo bungeni Mjini Dodoma alipokuwa akijibu hoja mbalimbali za wabunge kuhusu bajeti ya wizara yake, amesema kuwa Serikali inampango mkubwa wa kuwekeza hasa katika viwanda na sekta zingine mbalimbali.
“Niwaambie kitu ambacho kinakwamisha wawekezaji kuja Tanzania ni mazingira na udhaifu wa mapungufu ya TRA, mwekezaji makini hawezi kuwekeza sehemu ambayo kuna watu wengine wanalipa kodi mwingine halipi mwekezaji makini hawezi kuwekeza,”amesema Mwijage.