Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison George Mwakyembe leo Jumatano Mei 24, 2017 ataongoza viongozi na wanafamilia wengine wa michezo hususani wa mpira wa miguu kuilaki Serengeti Boys – timu ya soka ya Tanzania ya Vijana wenye umri wa miaka 17.

Serengeti Boys inatarajiwa kutua Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Julius Nyerere, Dar es Salaam, Tanzania leo saa 8:50 mchana kwa ndege ya Shirika la Ndege la Afrika Kusini ikitokea Libreville, Gabon kupitia Johannesburg nchini Afrika Kusini.

Mara baada ya kutua, timu itakwenda Hoteli ya Urban Rose kupata mapumziko angalau ya siku moja kabla ya TFF kuandaa utaratibu wa kuagana nao.

“Mpira huwa haulali, unachezwa saa 24 katika wiki duniani ambako huanzia Januari hadi Desemba, likimalizika shindano hili linakuja jingine. Maumivu ya kufungwa huwa ni mafupi, mashabiki siku zote huwa wanafkiria mechi ijayo. Tujiandae na Qulifiers za 2019 AFCON u-20, haziko mbali.” amesema Malinzi.

Timu hiyo ya vijana ilikuwa jijini Libreville nchini Gabon kushiriki fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika ya vijana iliyofanyika katika miji miwili ya Libreville na Port Gentil ambako iliondolewa kwenye hatua ya makundi na Niger.

 

Trump Akutana na Papa Francis, Mvutano wa Kujenga Ukuta Wamulikwa
Breakingnews: Rais Magufuli amtumbua Waziri Muhongo