Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri amewataka vijana kumcha Mungu kwa kuwasikiliza na kutii maelekezo yanayotolewa na viongozi mbalimbali ikiwemo vingozi wa dini ili kujenga jamii yenye maadili mema na yenye hofu ya kufanya mambo ambayo ni kinyume na maagizo ya Muumba wa mbingu na nchi.
Ameyasema hayo wakati wa mkutano wa hadhara na wachimbaji wadogo wadogo kwenye maeneo mbalimbali wilayani Sikonge, amesema kuwa siyo vyema kutumia maneno ya vijiweni kuyafanya ndio muongozo wa maisha ya kila siku, jambo ambalo linaweza kusababisha umwagaji damu.
Mwanri amesema kuwa utajiri unapatikana kwa mtu kufanyakazi kwa bidii na kwa kumtanguliza Mwenyezi Mungu katika kila kazi halali anayoifanya na kuongeza kuwa Serikali haina dini lakini inatambua kuwa wananchi wake wana dini zao.       
Hata hivyo, Mkuu huyo wa mkoa amewaonya baadhi ya vijana na watu wengine wasiendekeza maneno ya vijiweni ambayo yanaweza kuwajengea fikira potofu za kudhani mafanikio katika maisha yapatikana kirahisi na hivyo wengine kushinda wakicheza drafiti, bao , Pool badala ya kufanyakazi.

Sakata la Njiwa Kusafirisha Dawa za Kulevya Lamuibua Kamishna Mzowa
Mourinho kuvuta majembe mapya Manchester United