Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imetoa somo la masuala ya kodi kwa wafanyabiashara kutoka China wanaoishi nchini kwa lengo la kuwaongezea uelewa juu ya sheria na taratibu za ulipaji kodi.
Semina hiyo imefanyika jijini Dar es salaam ambapo imewajumuisha wafanyabiashara kutoka nchini china ambao wanafanya shughuli zao hapa nchini.
Aidha, Meneja wa Idara ya Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi wa TRA, Gabriel Mwangosi amesema kuwa Tanzania ya sasa ina fursa nyingi za uwekezaji hivyo wafanyabiashara hao watakapokuja kuwekeza lazima wafahamu kanuni na taratibu za ulipaji kodi nchini ili waweze kuendana na sheria zilizopangwa na nchini.
“Semina hii mahususi imeandaliwa kwa ajili ya wafanyabiashara wa kichina wanaoishi nchini kupata mafunzo ya kodi zikiwemo za zuio, majengo pamoja na ushuru na forodha ambazo ni lazima wazifahamu kwa manufaa ya Taifa letu na wao pia,”alisema Mwangosi.
Hata hivyo, Mwangosi ameongeza kuwa hii ni mara ya 6 kufanyika kwa semina hizo kwa wafanyabiashara hao ambapo tangu zianze kufanyika zimewasaidia kutokwenda kinyume na taratibu zilizowekwa nchin