Kiongozi wa zamani wa kijeshi wa Panama, Jenerali Manuel Antonio Noriega, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 83, mara baada ya kufanyiwa upasuaji wa kichwa katika hospitali ya Taifa ya nchi hiyo.
Aidha, Noriega amefariki dunia mara baada ya kufanyiwa upasuaji huo hivi karibuni ambapo ulipelekea kuvuja damu nyingi iliyopelekea hali yake kubadilika ghafla na kupoteza maisha.
Katika enzi za uhai wake Noriega alikuwa mshirika mkuu wa Marekani lakini baadaye Marekani ilimgeuka mara baada ya kuivamia nchi hiyo kisha kumtoa madarakani kwa nguvu mwaka 1989.
Hata hivyo, Noriega alifungwa jela kwa tuhuma mbalimbali yakiwemo makosa ya kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya na utakatishaji pesa, mauaji, ufisadi, na wizi wa mali za umma.