Meneja wa klabu ya soka ya Uingereza ya Arsenal, Arsene Wenger amekubali kuendelea kuifundisha klabu hiyo kwa kipindi cha miaka miwili zaidi.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka vyombo vya kuaminika, hatua hiyo imefikiwa baada ya kikao cha jana kati ya Babu Wenger na mmiliki wa klabu hiyo, Stan Kroenke ambapo alimwambia kuwa ataendelea na kazi yake kwa kipindi cha miaka miwili.
Arsenal imepanga kutoa tamko rasmi kuhusu kuongezwa muda wa miaka miwili kwa mkataba wa Wenger Jumatano wiki hii. Mkataba wake ulitarajiwa kuisha mwezi ujao.
Licha ya kukataliwa mara kadhaa na mashabiki, Wenger amemaliza kwa mafanikio ya aina yake kwa kubeba kombe la FA baada ya kutembeza kichapo cha 2-1 dhidi ya Arsenal katika uwanja wa Wembley Jumamosi iliyopita. Hata hivyo, alimaliza katika nafasi ya tano kwenye Ligi Kuu ikiwa ni mara kwanza kumaliza akiwa nje ya nafasi nne za juu tangu alipojiunga na timu hiyo mwaka 1996.