Mshindi wa tuzo tano kwa mkupuo za KTML mwaka 2011, 20 Percent haonekani kwenye ulimwengu wa muziki kutokana na harakati za kutaka kuingia mikononi mwa wasimamizi wapya wa muziki wake, imebainika.
Meneja wa msanii huyo, mtayarishaji wa muziki Man Walter amesema kuwa kuna watu waliotaka kumtoa mikononi mwa usimamizi wake na kwamba mchakato huo ndio uliopelekea kushindwa kurejea kwa kasi iliyokuwa ikitarajiwa.
“Unajua kuna jamaa walikuja kutaka kumsimamia 20% akanishirikisha nikamwambia hao jamaa inabidi watokee kwangu ili niweze kuwakabidhi nyimbo alizofanya na kuwaelekeza nini cha kufanya. Lakini nafikiri ni watu ambao walitaka kujaribu, sidhani kama wanauwelewa muziki vizuri,” Man Walter anakaririwa na Dizzimonline.
Hata hivyo, Man Walter alisisitiza kuwa bado 20 Percent yuko chini ya usimamizi wake na bado wanajendelea na mkakati wao.
Man Walter na 20 Percent waliteka spika zote muhimu kwa albam iliyobatizwa jina la ‘Mtanzania’ iliyoweka rekodi ya aina yake mitaani. Ilikuwa na nyimbo kama ‘Nimekusamehe’, ‘Mama Neema’, ‘Ningekusamehe’, ‘Why’ na nyingine.