Mbunge wa Arusha mjini, Godbless Lema amewataka viongozi waliopo Serikalini kuacha kufanya kazi kwa sifa na kutafuta kiki kwani wataliangamiza taifa.

Ameyasema hayo bungeni mjini Dodoma alipokuwa akichangia hoja katika bajeti ya wizara ya fedha, ambapo amesema kuwa kauli zinazotolewa na viongozi wa juu ni tishio kwa wafanyabiashara kwa sababu mazingira ya uwekezaji yamekuwa magumu.

Lema ameongeza kuwa kauli za vitisho kwa wafanyabiashara zitapelekea kuua uchumi wa nchi kwani watahamisha fedha na kuogopa kuwekeza nchini kitu ambacho kitazoofisha ukuaji wa uchumi wa nchi.

“TRA wamekuwa wakikusanya kodi wakiwa wameongozana na polisi, nawahakikishia hamtajenga uchumi imara katika nchi hii kwa kutanguliza ukali badala ya kuwa rafiki wa wafanyabishara,”amesema Lema

Mayweather aponda muziki wa Rap, awachana marapa wa sasa
Magazeti ya Tanzania leo Mei 31, 2017