Bunge nchini Marekani limetaka wakili wa Rais wa nchi hiyo, Donald Trump ahojiwe kufuatia sakata la Urusi kuingilia uchaguzi mkuu uliopita wa nchi hiyo.

Bunge hilo limefikia hatua hiyo mara baada ya wakili huyo kukataa kuhusishwa na uchunguzi huo wa bunge la Congress na lile la Seneti kuhusu suala la mawasiliano na Urusi.

Aidha, kwa upande wake, Michael Cohen ambaye ndiye wakili wa Trump amesema kuwa alikataa kuhusishwa na sakata la uchunguzi huo kwakuwa masuala hayo ni makubwa na hana uwezo wa kuyazungumzia.

”Nilikataa mwaliko huo kushiriki kwa kuwa wito wenyewe ulikuwa umetafsiriwa vibaya, ukigusia mambo mengi ambayo sina uwezo wa kuyakujibu”, aliambia chombo cha habari cha ABC katika mahojiano.

 

 

Manchester United klabu ghali kuliko zote barani Ulaya
Nyalandu aeleza mapya ya watoto majeruhi wa ajali ya Karatu waliopelekwa Marekani